loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ligi daraja la pili Dar yazidi kunoga

Uwanja wa Bandari kutakuwa na timu za Zakhem itakayomenyana na New Mzinga, Uwanja wa Mizinga Kigamboni utakuwa na mechi ya timu za Shababi na Tua Moyo.

Kwenye uwanja wa Kinesi kutakuwa na timu za Sinza Stars na Abajalo maarufu kama mnyama mkubwa huku Uwanja wa Airwing Ukonga kutakuwa na timu za Moro United na Sharif Stars.

Pia ligi hiyo itaendelea tena kesho ambapo Uwanja wa Bandari, Temeke Squad itawaalika Sifa Politan zote za Temeke na uwanja wa Airwing utakuwa na timu za Boom FC na Ukonga United zote za Ilala.

Katika uwanja wa Mwalimu Nyerere, timu ya Mshikamano itamenyana na Navy SC huku Uwanja wa Mizinga Kigamboni utakuwa na timu za Jamaica ya Mbagala na Panama.

Akizungumza Dar es Salaam, Katibu wa DRFA, Msanifu Kondo alisema anazishukuru timu kwa nidhamu waliyoonesha kwani hadi sasa hakuna malalamiko yaliyowasilishwa katika ofisi yake.

“Ligi tangu ianze imekwenda vizuri hivyo nazipongeza timu kwa nidhamu na naamini katika ngwe iliyobakia watadumisha nidhamu ili ligi imalizike katika muda muafaka, kwani TFF inataka majina ya washindi wa mikoa yawasilishwe Machi 30, mwaka huu”, alisema Kondo.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi