loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Lipumba alikataa kutii amri halali’

Zacharia alitoa madai hayo jana wakati akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha katika kesi ya kufanya maandamano bila kibali inayomkabili Profesa Lipumba na wafuasi wake 30.

Alidai kuwa Januari 26 mwaka huu, waliona tangazo la CUF kufanya maandamano na mkutano Januari 27, katika eneo la Mbagala Zakhem kupitia kwenye vyombo vya habari, hivyo aliwatuma askari wafuatilie taarifa hizo. Zacharia, ambaye wakati huo alikuwa Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, alidai siku hiyo katika mtaa wa Boko, karibu na hospitali ya Temeke na Benki ya NMB, askari waliokuwa katika eneo hilo walimpa taarifa kuwa watu wameanza kukusanyika katika eneo hilo.

Alidai, wakati huo hakuwa na taarifa za maandishi kuhusu jambo hilo, hivyo aliwasiliana na Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro ambaye alimwambia CUF waliandika barua kuhusu kufanya maandamano na mkutano lakini wamezuia kufanya maandamano hayo na akatumiwa nakala ya zuio hilo.

Aliendelea kudai kuwa taarifa aliyopewa ilionesha kwamba katika mkusanyiko huo ‘haramu’ Prof Lipumba alikuwepo pamoja na wafuasi wake wakiwa wameshika vipeperushi vya bendera za CUF na mabango.

Alisema baada ya nusu saa, walianza kuondoka kupitia barabara ya Sudan hadi Mtongani wakiwa katika kundi la watu wanaokaribia 200. Alidai alienda eneo la tukio na kumwambia Lipumba kuhusu zuio hilo ambaye alikiri kupokea barua ya zuio hilo.

“Nilimsihi wasifanye maandamano, watii zuio la polisi na kama hawajaridhika wakate rufaa kwa Wiziri ya Mambo ya Ndani lakini alikaidi huku wafuasi wake wakiwatukana askari na kuwaita vibaraka wa CCM,” alidai.

Alidai waliwasiliana na Siro ambaye alisema, watumie taratibu za kuwazuia kwa mujibu wa sheria, hivyo walitoa ilani mara tatu ili watawanyike baada ya muda kupita waliwakamata watu 31 na kwamba katika ukamataji huo walitumia nguvu ya kawaida.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi