loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lugha chafu Chalinze zamkera Lubuva

Mwenyekiti wa NEC, Damiani Lubuva alisema hayo leo Dar es Salaam alipokuwa akitangaza tarehe ya uchaguzi huo wa Chalinze utakaofanyika Aprili 6 mwaka huu.

Alisema Tume imekuwa ikifuatilia kampeni hizo ambazo zimekuwa zikifanywa katika maeneo mbalimbali na vyama vya siasa vilivyosimamisha wagombea kwa kuzingatia ratiba iliyowekwa na msimamizi wa uchaguzi.

“Tunasikitishwa na lugha hizo ambazo wakati mwingine zimekuwa zikihamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi au kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa lengo la kuwazuia wasishiriki uchaguzi huo,” alisema Lubuva bila kutaja vyama husika.

Aidha alitaka vyama kuzingatia sheria , kanuni, taratibu na maadili ya chaguzi yaliyokubaliwa na vyama vyote vya siasa.

“Lugha za kejeli zisizo na staha, vitisho na kuzuia wapiga kura kushiriki uchaguzi ni ukiukwaji wa sheria hivyo yeyote atakayebainika amekiuka na kuvunja sheria atachukuliwa hatua za kisheria,” aliongeza Lubuva.

Alitaka vyama kuepuka kuchukua sheria mkononi kwa kuadhibu watu wanaodaiwa kuvunja sheria badala yake, wawakabidhi kwenye mamlaka za kisheria.

Aliongeza Tume inatarajia kuona kwamba kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura katika Jimbo la Chalinze anatumia haki yake ya kikatiba na sheria kupiga kura kwa amani na utulivu pasipo vitisho wala kubugudhiwa.

Vyama vilivyosimamisha wagombea (katika mabano) ni Chama Cha Mapinduzi (Ridhiwani Kikwete); Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Mathayo Torongey) na Chama cha Wananchi ( Fabiani Skauki).

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi