loader
Picha

Lukaku avunja rekodi ya usajili Everton

Mchezaji huyo akiwa na timu hiyo aliifungia mabao 16, amesaini mkataba wa miaka mitano na Everton akitokea Chelsea.

Kocha wa Everton, Roberto Martinez alisema hatua ya kumsajili mchezaji huyo ni ya kimafanikio kwa kiasi kikubwa kwa kuwa atakuwa msaada kwa klabu hiyo.

Lukaku alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Anderlecht kwa kitita cha Pauni milioni 18 kunzia Agosti 2011 na aliichezea michezo 15 tu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wake huo, Lukaku alisema amekuwa na furaha kubwa kusajiliwa na Everton.

Alisema akiwa na miaka 21, kwake ni fursa kubwa kuitumikia kwa hali na mali klabu hiyo ambayo kwake anaona ni kama amerejea nyumbani.

Lukaku ameipiku rekodi ya usajili ya mchezaji Marouane Fellaini wakati akijiunga na klabu hiyo akitokea Klabu ya Standard Liege mwaka 2008 ambapo alichukuliwa kwa kitita cha Pauni milioni 15.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi