Kutokana na changamoto hizo, kunawalazimisha mara kadhaa kutoa taarifa zinazoelezea mwenendo wa mabadiliko hayo na tahadhari kwa wananchi.
Hata hivyo alisema, mamlaka ya hali ya hewa imeendelea kutoa taarifa zinazotolewa kuwa na mafanikio makubwa kwa wananchi kwa kusaidia kupunguza majanga mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu huyo alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa juzi mara baada ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Festo Kiswaga, kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo ambacho pia kilikuwa na jukumu la kupitisha bajeti ya mwaka 2015/2016.
Hivyo alisema kutokana na mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa ni vyema wananchi wakawasiliana na maofisa ugani ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu kilimo chao kulingana na mvua zilizopo.