Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kwanza ya kutembelea Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) tangu alipoteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri huyo alisema ana imani kubwa na utendaji wa TNBC na atahakikisha anashirikiana na watendaji wake kuendelea kujenga mazingira bora ya biashara na kuyawezesha mabaraza ya mikoa ya biashara.
“Tunahitajika kuendelea kujenga mazingira bora ya kufanya biashara na kuyawezesha mabaraza ya biashara ya mikoa yaweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu taratibu zake,” alisema.
Alisema TNBC ina wajibu wa kuhakikisha inafanya kazi karibu na mabaraza ya mikoa na wilaya ili kuzidi kujenga mazingira bora ya biashara.
Waziri huyo alifanya ziara ya kutembelea baraza hilo, kujionea shughuli zake na kujifunza zaidi juu ya utendaji wake.