loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mabonde ya maji yafaa yatunzwe

Ili kuhakikisha kuwa mabonde hayo yanasimamiwa vyema, serikali ilifungua ofisi katika mabonde hayo na kuweka mikakati endelevu ya upatikanaji wa maji. Ofisi ya kwanza ilifunguliwa katika Bonde la Mto Pangani mwaka 1991.

Bonde la hilo lipo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania na linapita katika wilaya 17 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.

Bonde hilo lina mabonde madogo katika mito mikubwa ya Pangani, Zigi, Umba, Mkulumuzi na Msangazi, ambayo inamwaga maji katika Bahari ya Hindi.

Bonde la Pangani pia linajumuisha mabonde yanayotitirisha maji kutoka milima ya Kilimanjaro, Meru, Usambara na Upare. Aidha, bonde hilo linajumujisha maji ya ziwa Chala, Jipe, Duluti na Karamba na mabwawa ya Nyumba ya Mungu, Mabayani na Kilimawe.

Bonde lingine ni la Mto Rufiji, ambalo lilipata ofisi ya maji mwaka 1993. Bonde hilo linajumusha eneo lote, ambalo mwelekeo wa maji yake huingia Mto Rufiji, kisha kumwagwa katika Bahari ya Hindi.

Bonde la Rufiji lina mito mikuu ya Ruaha Mkuu, Kilombero na Luwegu. Lingine muhimu ni Bonde la Ziwa Victoria ambalo lilipata ofisi ya maji mwaka 2000.

Bonde hilo liko ndani ya Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika. Mito inayomwaga maji yake katika Ziwa Victoria ni Kagera, Simiyu, Mbarageti, Gurumeti, Mara na Mori.

Ni dhahiri kuwa mabonde haya ni rasilimali kubwa ya taifa na yanatakiwa yatunzwe kikamilifu. Mabonde haya yote na mengineyo, yamekuwa yakitumika kwa miaka mingi kwa matumizi mbalimbali, kama vile uzalishaji wa umeme.

Kwa mfano, Bonde la Mto Pangani, lina mabwawa ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia nguvu ya maji, ambayo ni Pangani na Nyumba ya Mungu, wakati katika Bonde la Mto Rufiji kuna mabwawa ya kuzalisha umeme ya Mtera, Kidatu na Kihansi.

Pia, mabonde hayo yanajumuisha mito inayotumiwa kwa shughuli za usafiri na uvuvi. Mabonde yanayotumika kwa usafiri na uvuvi ni kama Pangani na Rufiji. Faida nyingine kubwa ya mabonde hayo ni kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa viwandani.

Kwa mfano, bonde la mto Rufiji na bonde la mto Kilombero yanatumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Ni dhahiri pia kuwa mabonde hayo tisa, yanayohifadhi maji mengi, yametengeneza mandhari nzuri, zinazovutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.

Kila mwaka maelfu ya watalii kutoka nje ya nchi, hutembelea mabonde hayo hivyo kuiingizia serikali fedha nyingi za kigeni. Kinachotakiwa kufanywa kwa sasa tushirikiane sote kutunza mabonde hayo ili yaendelee kunufaisha vizazi vingi vijavyo.

Tupige vita uharibifu wa aina yoyote wa mazingira katika mabonde hayo. Kila mtu anapaswa kuheshimu vyanzo hivi vya maji, kutokana na ukweli kwamba ‘bila maji hakuna uhai’.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi