loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Madaktari muwe wazalendo'

Mbunge huyo alihoji mikakati ya Serikali katika kuhakikisha madaktari wanaosomeshwa wanabaki hapa nchini na si kukimbilia nje ya nchi.

Akijibu swali hilo, Waziri Ghasia alisema Sera ya Maslahi na Motisha katika utumishi wa umma ni miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.

Alisema madaktari wanatakiwa kuwa na uzalendo na kuangalia maslahi ya nchi yao kwani tofauti ya maslahi ni kidogo sana kwa madaktari wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi. Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Betty Machangu (CCM) alisema wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini wamejenga zahanati 41 na vituo sita vya afya.

Mbunge huyo aliuliza lini Serikali itapeleka madaktari katika zahanati hizo pamoja na magari ya wagonjwa, mashine za X-ray na vifaa vingine vya tiba? Akijibu swali hilo, Waziri Ghasia alisema Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ina upungufu wa watumishi katika kada za afya wapatao 88 na waliopo ni 141.

Alisema moja ya changamoto inayoikabili sekta ya afya ni uhaba wa watumishi ambao kwa sasa unafikiwa wastani wa asilimia 40 nchi nzima. Hata hivyo Serikali kila mwaka hupanga watumishi wake wa kada hiyo kadri wanavyohitimu na kufaulu mafunzo katika vyuo vya afya.

Alisema katika mwaka 2012/13 Serikali ilipanga watumishi wa afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wapatao 14 ambapo kati ya hao watabibu ni 13.

Pia alisema katika mwaka 2013/14 halmashauri hiyo imeomba kibali cha kuajiri watumishi wengine 88 na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila kituo cha afya kinakuwa na gari la kubebea wagonjwa.

Alisema mpaka sasa vituo vya afya vyenye magari ya kubebea wagonjwa ni Kirua Vunjo na Mwika hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi inashauriwa kutenga fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kununua magari hayo kwa vituo vya afya vilivyobaki.

Akizungumzia suala la mashine za X-ray na utra sound alisema Serikali kwa sasa inaendelea kukamilisha ujenzi wa chumba cha X-ray katika hospitali mpya ya wilaya , Himo inayojengwa katika Mji wa Himo.

Pia aliziagiza halmashauri zote ikiwemo Halmashauri ya Moshi kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi