loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madeni ya ATCL yabakia bil. 40/-

Katika hatua nyingine, kuboreshwa kwa mazingira ya biashara ya anga nchini, kumefanya mashirika makubwa ya ndege duniani kuomba ndege zao kutua mara tatu nchini kutoka mara moja kwa siku ilivyokuwa nyuma.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alipokuwa akitoa majumuisho kwenye Hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2015/2016, uliopitishwa na Bunge juzi jioni.

Akizungumzia juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha Sekta ya Usafiri wa Anga, Dk Tizeba alisema kuna juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kufanya sekta hiyo kuwa bora kwa kuboresha mazingira yenyewe lakini pia kuiboresha ATCL.

Alisema deni kubwa lililokuwa linaikabili ATCL lilikuwa kikwazo kikubwa katika kulifanya kufufuka na kutoa ushindani, lakini kazi kubwa imefanywa katika kurekebisha Mizania ya Madeni kutoka Sh bilioni 133 hadi Sh bilioni 40 na kuna uwezekano wa kiasi kilichosalia nacho kupungua.

“Suala hili na madeni lilikuwa kikwazo kikubwa katika kuvutia uwekezaji ndani ya ATCL. Hata hivyo, hali sasa imezidi kuimarika na kama fedha zilizotumika katika uwekezaji ndani ya TRL (Shirika la Reli Tanzania) tungezitumia katika kununua ndege tungeweza kupata ndege kati ya 10 na 15,” alisema Dk Tizeba.

Kuhusu kuboreshwa kwa mazingira ya usafirishaji wa anga, alisema hali sasa imekuwa rafiki kuliko ilivyokuwa awali hatua iliyofanya kampuni kubwa za ndege duniani kuomba kutua nchini mara tatu kwa siku kutokana na kuridhishwa na mazingira yaliyopo.

Alisema kazi nyingine inayofanywa na serikali sasa ni kuboresha viwanja vikubwa vinne vya ndege nchini vya Julius Nyerere (JNIA), Songwe, Mwanza na Kilimanjaro (KIA).

Alisema kwa upande wa JNIA, ujenzi wa Kiwanja cha Tatu cha Ndege (Terminal 3) unaendelea na lengo ni kuhakikisha kuwa unamalizika ifikapo Novemba mwakani huku akisema fedha za ujenzi zipo.

Alisema ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Mwanza unaendelea kwa kuweka tabaka la pili la lami lenye ujazo wa mita 500 na Songwe kinachofanyika ni ujenzi wa jengo la kisasa la mapumziko ya abiria.

UMOJA wa Ulaya (EU), Norway na Sweden wametoa Dola za ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi