loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madiwani wakutana kwa mkopo

Aidha, wametoa siku 30 kwa halmashauri kuhakikisha vyanzo vya mapato vinasimamiwa vizuri.

Katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika mjini hapa, kilichokuwa na ajenda ya kunusuru hali ya kifedha iliyopo kwenye halmashauri hiyo, madiwani waliazimia vikao na ofisi kuendeshwa kwa mikopo.

Baadhi ya madiwani hao akiwemo wa Kata ya Mwaubingi, Sayi Mwangubisia alisema kuwa chanzo kikubwa kuwepo kwa ukata wa fedha katika halmashauri yao ni mfumo mpya wa ukusanyaji ushuru wa pamba.

“Awali halmashauri ndiyo ilikuwa inakusanya ushuru wa pamba…kwa sasa Bodi ya Pamba ndiyo inakusanya na hizo fedha sasa hivi zinaenda moja kwa moja hazina na kuzipata fedha hizo hadi Oktoba au Novemba, unafikiri hapa katikati nini kitafanyika? ” Alihoji Mwangubisia.

“Tumeamua kwa hali hii, vikao vyote vya utekelezaji pamoja na uendeshaji wa ofisi viendeshwe kwa watu kukopwa na fedha zikija watu watalipwa lakini kuna baadhi ya vikao havitafanyika maana madeni yatakuwa mengi na kuna hatari miradi kushindwa kutekelezwa kutokana na vikao vya kupitisha kutofanyika,”alisema diwani huyo.

Hata hivyo madiwani hao katika kikao hicho waliitupia lawama Idara ya Fedha kwa kushindwa kusimamia ipasavyo vyanzo vingine vya mapato ikiwemo magulio, pamoja na uuzaji wa nafaka, kutokana na makusanyo ya vyanzo hivyo kuwa chini ya kiwango.

Walisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakichukua mahindi, maharage, dengu pamoja na kunde ndani ya halmashauri hiyo bila ya kulipia ushuru hali inayochangia kushindwa kujiendesha.

Pia walitoa siku 30 kwa idara hiyo kuhakikisha vyanzo hivyo vinasimamiwa kwa kiwango kwa nguvu huku wakitaka ndani ya muda huo kuletewa takwimu sahihi za ukusanyaji wa ushuru katika vyanzo hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Magamula Mabula alikiri halmashauri hiyo ipo katika hali ngumu kutokana na kutokuwa na fedha, huku akikiri kuwa vikao pamoja na ofisi vinaendeshwa kwa mkopo. Asilimia 40 ya pamba inazalishwa mkoani Simiyu.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Bariadi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi