loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mafia kuunganishwa katika gridi ya Taifa

Kitwanga alisema kuwa kwa hivi sasa, wizara iko kwenye hatua ya utafiti wa jinsi ya kutandika nyaya baharini.

“Wizara iko kwenye utafiti wa kuangalia jinsi ya kutandika nyanya za umeme baharini ili tuiunganishe wilaya hii katika gridi ya taifa…tatizo moja ambalo inabidi tukabiliane nalo ni kuwa hapa kuna kina kirefu sana cha maji kuliko kule Zanzibar,” alisema Kitwanga.

Akizungumzia usambazaji wa umeme unaofanywa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Kitwanga alisema katika awamu ya pili ya mpango wa REA, serikali haitalipa fidia katika kupisha usambazaji wa umeme ili watu wengi wapate umeme.

Alisema katika awamu ya kwanza, Serikali ililipa fidia kwa wananchi, jambo ambalo lilifanya vijiji vichache vipate huduma hiyo muhimu kwa sababu kiasi kikubwa cha fedha, kilitumika kulipa fidia badala ya kugharamia mradi.

“Katika awamu ya kwanza tulilipa fidia, ila tulijifunza, kutokana na kulipa fidia tuliweza kupekeka umeme sehemu chache kwa sababu sehemu nyingine gharama ya kufidia ni kubwa kuliko gharama ya kusambaza umeme,” alisema na kuongeza:

“Serikali imeweka sera kwamba katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi, mahali ambapo tutapeleka umeme wa REA hatutatoa fidia, hivyo huo utakuwa ni mchango wa wananchi katika kutekeleza mradi.”

Alisema baada ya Serikali kuondoa fidia, imeamua kupunguza gharama za kuunganisha umeme kuwa Sh 27,000 badala ya Sh 177,000, na kuwa tofauti ya gharama hiyo ambayo ni Sh 150,000 italipwa na Serikali.

“Hapo usiseme hatujafidia, ni kuwa tumetoa fedha huku na kupeleka huku,” alifafanua.

Alisema vijiji vinne, vikiwemo Jibode, Chole na Bwejuu ambavyo havipo kwenye mpango wa REA, Wizara inaangalia namna ya kuwaunganisha na umeme jua. Kitwanga alisema Wilaya ya Mafia, itapata umeme huo kwa asilimia 100, kutokana na vijiji vyake vyote kupata umeme katika awamu ya pili.

Alitaka wananchi kushiriki ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Kitwanga alisema, gharama ya kutekeleza mradi wa REA katika Wilaya ya Mafia ni sh bilioni 5.7 huku gharama ya kuzalisha umeme huo ikiwa ni zaidi sh milioni 400 kwa mwezi.

“Gharama kuzalisha umeme kwa Mafia ni zaidi ya Sh milioni 400, lakini makusanyo ya wakazi wa Mafia kwa sasa ni sh milioni 80. Kama lengo la Serikali lingekuwa ni kusambaza umeme kwa faida, basi Mafia isingepata umeme, ila haijawa hivyo kwa sababu Serikali yenu inawajali,” alisema.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi