loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mafunzo waichapa Kizimbani

Mafunzo ambao huo ulikuwa mchezo wao wa kumalizia ratiba, imemaliza ligi hiyo ikiwa na pointi zake 32 katika msimamo wa ligi hiyo ambayo bado inaongozwa na Polisi yenye pointi 40.

Katika mchezo huo, Kizimbani ndio waliotangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 29 lililofungwa na mchezaji wake Juma Rashid na Mafunzo kusawazisha katika dakika ya 38, bao lililofungwa na Wahid Ibrahim.

Miamba hiyo ambayo ilikuwa ikishambuliana kwa zamu ilimaliza dakika 45 za awali, kukiwa hakuna aliyeweza kuuona mlango wa mwenzake.

Kuanza kwa kipindi cha pili kila mmoja ilijirekebisha makosa yake na Mafunzo ikaongeza bao la pili lililofungwa na mchezaji Ibrahim katika dakika ya 61 na kuongeza bao la tatu katika dakika ya 75 lililofungwa na Rashid Kariha.

Kizimbani ambao walionekana kutokata tamaa walijitahidi kuliandama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 78 lililofungwa na mchezaji wake Khatib Hassan na kuufanya mchezo huo umalizike kwa Mafunzo kushinda mabao 3-2.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo katika uwanja wa Amaan kwa mchezo kati ya Malindi na Jamhuri.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi