loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magereza, Mabuloya wang’ara ngoma za asili za Balimi

Kumalizika kwa mashindano hayo kunakwenda sambamba na mikoa hiyo kupata wawakilishi wake katika fainali za mashindano hayo ngazi ya taifa zinazotaraji kuanza Mwanza leo.

Katika Mkoa wa Tabora, kikundi cha Magereza Arts Group kilinyakua ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu Sh 600,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali za Kanda.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Bugobogobo na ambayo ilizawadiwa fedha taslimu Sh 500,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za Kanda.

Vikundi vinane ambavyo ni JKT, Hekima, Uvikuja, Wembe Group, Hiari ya Moyo, Zugo Group vilishiriki mashindano hayo.

Mkoa wa Shinyanga kikundi kilichochukua ubingwa ni Mabuloya Jeshi ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Sh 600,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za Kanda.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Wananguli Bugumbagu ambao walizawadiwa fedha taslimu Sh 500,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga kwenye fainali za Kanda jijini Mwanza.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi