loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mahakama ya Kadhi yatoa elimu kwa wanandoa

Mahakama ya Kadhi yatoa elimu kwa wanandoa

Elimu hiyo ni pamoja na kufahamu haki zinazopatikana kwa watu wawili wanaofunga ndoa kwa lengo la kupambana na tatizo la talaka zinazotolewa ovyo. Akizungumza na gazeti hili, Ngwali alikiri kuwepo kwa talaka nyingi zinazotolewa ovyo.

Alisema hivi sasa wanaume wengi wanatumia talaka kama silaha ya kuwadhalilisha wanawake kwa kuwatisha kuwaacha.

“Tumeanza kutayarisha programu maalumu ya vipindi katika Televisheni na Redio kutoa elimu kuhusu athari za talaka na wakati gani talaka inatakiwa itolewe katika masharti yapi...tumegundua wanaume wanatoa talaka ovyo,” alisema.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2012 hadi Septemba mwaka 2013, zaidi ya talaka 50 zimetolewa kwa upande wa mkoa wa Mjini Magharibi katika Mahakama ya Kadhi Mwanakwerekwe na Mwera.

Alitaja athari kubwa za wanaume wanapotoa talaka ni kusambaratika kwa watoto, ambao wanakosa matunzo mazuri ya baba na mama.

Aidha, alisema talaka ndiyo chanzo cha watoto wengi kuwa ombaomba barabarani pamoja na wengine kujiingiza katika ajira ngumu kwa ajili ya kujipatia kipato baada ya kukosa matunzo mazuri ya wazazi wawili.

“Hizo ndiyo athari za talaka zinazotolewa bila ya kuzingatia maadili na Sheria ya Ndoa... tunapokea malalamiko mengi ya wanawake kutelekezwa pamoja na watoto katika Mahakama za Kadhi,” alisema.

Kadhi wa Mahakama ya Wilaya Mkokotoni ambaye hufanya kazi zake pia katika Mahakama ya Kadhi Mfenesini, Khamis Kassim Haji alisema kesi za wanawake kudai matunzo ya watoto na wao kutelekezwa, zimekuwa nyingi na ndiyo chanzo cha kuwepo kwa talaka.

Alisema katika Mahakama ya Mkokotoni katika mwaka 2012 jumla ya talaka 53 zilitolewa baada ya wanandoa kushindwa kufikia suluhu ya matatizo yao.

Alisema hali hiyo ilisababisha watoto wengi kukosa matunzo ya wazazi wawili. “Kesi za wanawake kutelekezwa na waume zao, watoto kukosa matunzo na talaka zimekuwa zikiongezeka kwa wingi katika mkoa wa Kaskazini wenye idadi kubwa ya wananchi Unguja,” alisema.

Haji alisema ana matumaini makubwa kwamba kukamilika kwa Rasimu ya Mahakama ya Kadhi, kwa kiasi kikubwa itapunguza matatizo mbali mbali ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, vinavyolalamikiwa na wanawake, ikiwemo kutelekezwa na kushindwa kupata mgawanyo wa mali wakati wanapoachwa.

“Tunaisubiri rasimu ya sheria ya Mahakama ya kadhi ambayo kwa kiasi kikubwa itakapokamilika itapunguza malalamiko ya wanawake na kupunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia,” alisema.

Utafiti mdogo uliofanywa na TAMWA unaonesha kwamba wanawake wanatelekezwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutokana na wanaume wengine kuoa wake zaidi ya wawili na hivyo kushindwa matunzo ya mama na watoto.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi