Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aziza Kalli alitoa hati hiyo kwa kuwa mshitakiwa huyo jana hakufika mahakamani kwa ajili ya kusomewa hukumu ya kesi inayomkabili yeye na wenzake tisa.
Hakimu Kalli aliamuru Nyipembe akamatwe ili asome hukumu hiyo wakati washitakiwa wote wapo mahakamani.
Aliahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo atakapotoa hukumu hiyo.
Awali hukumu hiyo ilitakiwa kusomwa Juni 20 mwaka huu lakini iliahirishwa kwa kuwa mshitakiwa huyo wala wadhamini wake hawakufika Mahakamani bila taarifa.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kughushi na wizi wa kontena yenye vipuri chakavu vyenye thamani hiyo.
Inadaiwa waliiba kontena hilo lililokua linasafirishwa kwenda Lusaka, Zambia mali ya kampuni ya M/S Emmy Chris Investment ltd inayomilikiwa na raia wa Nigeria, Jude Nwizu.
Mbali na Nyipembe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Peter Mchonvu, Deo Asterio , Michael Harani, Salum Mohamed, Ally Abdallah, Richard Mramba , Josephat Ndashau, Mudithan Mpini na Amina Mgonja.