loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Majambazi washtukiwa wakitaka kupora benki

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishina wa Polisi Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao waliingia katika benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja waliobeba fedha nyingi lakini kumbe yalikuwa na mawe, kokoto na uchafu mwingine.

Alisema walipofika katika benki hiyo iliyopo mtaa wa Swahili, watuhumiwa watatu kati yao waliingia ndani ya benki hiyo wakiwa na mifuko hiyo na walinzi waliwapokea wakijua ni fedha na kuwasaidia hadi ndani.

“Watu hao walipoingia ndani walianza kulazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kawaida na kutaka kuingia kwa nguvu kwenda kupora fedha, lakini kwa vile benki hiyo ilikuwa na mitambo pamoja na ving’ora vya tahadhari vilianza kulia na kuwatia hofu wahalifu hao,” alisema.

Kova alisema wahalifu hao waliamua kutoka nje kwa kasi ambapo kulikuwa na gari aina ya Noah na pikipiki moja ambazo hazikusomeka namba kwa haraka na wakatoweka baada ya kufyatua risasi hewani na kuwatishia watu waliokuwa nje na ndani ya benki hiyo.

“Baada ya kuondoka majambazi hao iligundulika mmojawao alichota kiasi cha fedha ambazo mteja alizileta kwa madhumuni ya kuziweka katika tawi hilo. Walitelekeza mifuko yao iliyokuwa imejaa mawe, kokoto na uchafu mwingine waliokuwa wakidanganya kwamba ni fedha,” alisema.

Kutokana na tukio hilo alihimiza benki zote kuchukua tahadhari za kiusalama, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanaingia mkataba wa kulindwa na jeshi la polisi, kuweka vifaa mbalimbali vya ulinzi vitakavyobaini mtu anapoingia na silaha au kitu hatari.

“Tunajua benki zingine zinaogopa gharama lakini tunaamini benki zinazolindwa na polisi zinakuwa na usalama zaidi. Tutazungumza na Benki Kuu ili kuhakikisha benki zote zinalindwa na polisi na watakaokaidi tatizo linapotokea wawajibishwe,” alisema.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi