loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majambazi yamuua mfanyakazi wa TBC

Gize, ambaye alikuwa dereva wa shirika hilo, aliuawa usiku katika eneo la Ubungo Maziwa wakati akiwa kazini, akienda kuchukua wafanyakazi kuwapeleka kazini kwa zamu ya usiku.

Kulingana na taarifa kutoka TBC, alipigwa risasi akiwa ndani ya gari karibu na duka ambalo majambazi hao walikwenda kupora.

Ilielezwa ilikuwa kabla ya saa 6 usiku. Sanjari na dereva huyo, mtu mwingine, Mwarami Rajabu aliyekuwa jirani na duka hilo, alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na majambazi hao.

Gize ametumikia TBC kwa miaka saba tangu 2007. Msiba uko maeneo ya Ubungo Kibangu, wilayani Kinondoni kwa babake, Ismail Gize.

Mwili wake utaagwa leo katika Hospitali ya Mwananyamala kabla ya kusafirishwa kwenda Magole mkoani Morogoro kwa maziko. Alizaliwa Januari mosi 1968 na ameacha watoto watatu.

Taarifa ya habari ya TBC1 iliyomkariri Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, ilisema hadi jana hakuna aliyekuwa amekamatwa kuhusika na mauaji hayo. Hata hivyo, kamanda alisema wanaendesha msako kubaini wahusika.

MWENYEKITI wa Taasisi za Sekta Binafsi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi