loader
Dstv Habarileo  Mobile
Maji machafu, harufu kali tishio Soko Kuu Dodoma

Maji machafu, harufu kali tishio Soko Kuu Dodoma

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti sokoni hapo, walisema miundombinu iliyopo ya mifereji ya maji machafu, inahatarisha uwepo wa magonjwa ya mlipuko kwa wauzaji na walaji.

Pia, walisema hatari nyingine inayoweza kusababisha na mlipuko huo wa magonjwa ambapo hivi sasa soko hilo linatoa harufu kali na kuna dampo la takataka, ambalo lipo eneo linalouziwa mbogamboga.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Kanali Iddi ambaye ni muuza nazi alisema mazingira wanayofanyia biashara zao hivi sasa ni machafu kutokana na wingi wa takataka zinazozalishwa kwenye soko hilo ambalo linahudumia wakazi wa Dodoma na nje ya Mkoa.

Alisema kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha hali ni mbaya katika maeneo ya mazingira yaliyowekwa ya kibiashara ambayo wafanyabiashara walio wengi wamekuwa akipanga chini bila kujali maeneo hayo ni salama.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Afya soko hilo, Rhoda Boy alisema mazingira hayo ya uchafu pia yanachangiwa na akina mama lishe ambao kwenye maeneo yao ya kupigia vyakula hakuna miundombinu inayoweza kusafirisha maji hayo machafu.

Alisema hata mama lishe wamekuwa wakimwaga maji machafu hovyo kutokana na kukosa maeneo rasmi, na wanalazimika kwenda kumwanga kwenye mfereji ambao hata hivyo umegeuzwa kuwa kama jalala la takataka ambalo linatoa harufu kali sana.

Pia Makamu Mwenyekiti wa soko hilo, Abdallah Mchawi alisema kuwepo kwa uchafu katika soko hilo kuasababisha vitendea kazi vya kuzolea takataka kukosekana hali ambayo inayowafanya hata wafanyakazi kuzoa kwa kutumia mifuko ya sandarusi.

Alisema tatizo lililopo kwenye soko hilo ni wakala aliyepewa kazi ya kuzoa takataka wafanyakazi wake hawana vitendea kazi na walio wengi wanatumia mikono yao huku wakiwa wamevaa mikononi mifuko ya plastiki kuzoa uchafu.

Alisema kutokana na hali hiyo kwa asilimia mia moja ugonjwa wa kipindupindu utazuka wakati wowote isipochukuliwa hatua za haraka kujihami na hali mbaya iliyopo kwenye soko hilo.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi