loader
Picha

Makamu wa Rais Fifa afariki dunia

Grondoka ambaye amekuwa katika uongozi wa chama hicho tangu mwaka 1979, alizidiwa na ugonjwa juzi baada ya kupata mshituko wa moyo.

Kifo chake kilitangazwa na Shirikisho la Vyama vya Soka vya Amerika Kusini (CONMEBOL).

Wakati wa utawala wake katika AFA, Argentina ilifika mara tatu katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia, ikishinda mara moja mwaka 1986 kabla ya Ujerumani Magharibi kulipa kisasi miaka minne baadaye.

Mapema mwezi uliopita nchini Brazil, ilifika fainali ya 2014, kabla ya kufungwa kwa bao la muda wa nyongeza la Mario Gotze wa Ujerumani.

Utawala wake wa muda mrefu katika soka ulimfanya Grondona ashike wadhifa wa Makamu wa Rais Mwandamizi wa Fifa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chombo hicho cha juu cha soka duniani.

Rais wa Fifa, Sepp Blatter aliongoza mamia ya wapenda soka duniani kuomboleza kifo hicho, akisema:

“Ninasikitika kwa kumpoteza rafiki mkubwa. “Julio Grondona ametutoka katika umri wa miaka 82. Naipa pole familia yake. Apumzike kwa amani.”

Lionel Messi pia alieleza masikitiko yake kutokana na taarifa hizo, akiweka ujumbe katika mtandao wake wa Facebook: “Hakika ni siku ya huzuni kwa jamii ya soka, kwa Argentina na kwangu.

“Rais wetu wa AFA, Julio Grondona, ametutoka. Napenda kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia na marafiki wa mpendwa huyu.”

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: BUENOS AIRES, Argentina

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi