Mbali na Ngabo, karibu makocha wengine wote waliokuwa chini yake ukiwaondoa Mzonge Hassan na Khadija Manzi, wengine wote wameondolewa.
Makamu Mwenyekiti wa BFT, Lukelo Willilo alisema wamefanya mabadiliko hayo ili kupata maendeleo ya mchezo huo baada ya Ngabo kuiongoza timu hiyo kwa muda mrefu bila mafanikio.
Wengine walioondolewa ni Edward Emmanuel, Said Omary `Gogo Poa’, Richard Selenge na Juma Maisori.
Selemani ambaye ana jukumu la kuinoa timu hiyo kwa ajili ya Michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Scotland mwaka huu, atasaidiwa na Jonathani Mwakipesile pamoja na Mzonge na Manzi.
Naye Selemani akizungumza kwa simu na gazeti hili, alisema anasubiri ruhusa kutoka kwa mwajiri wake ili aanze kazi rasmi ya kuifundisha timu hiyo na ndipo atakuwa tayari kuzungumzia mikakati yake.