loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Makocha wasuasua kuwasilisha ripoti za Madola 2014

Akizungumza na 'Habarileo', Meneja wa timu hiyo Muharami Mchume alisema kocha wa ndondi, Jonas Mwakipesile ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha ripoti hiyo tangu wakiwa Glasgow.

Mchume alitaja michezo ambayo hawajawasilisha ripoti zao kwake ni baiskeli, judo na kuogelea wakati kunyanyua vitu vizito, mpira wa meza wameshawasilisha ripoti zao tayari.

Hata hivyo, kocha wa judo, Zaid Hamisi alisema jana kwa njia ya simu kuwa ripoti iko tayari na leo Jumapili anatarajia kuituma katika Kamati ya Ufundi ya Chama cha Judo (TAJA) kujadiliwa kabla ya kutumwa kwa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

“Ripoti iko tayari na kesho (leo) nitaituma TAJA ambao itajadiliwa na Kamati ya Ufundi kabla ya kuwasilishwa TOC, mimi nawajibika kwa chama changu kwanza,” alisema Zaidi.

Naye kocha wa baiskeli, Godfrey Mhagama alisema yuko Kahama na ripoti anayo, lakini ataiwasilisha Agosti 27 baada ya kurejea Dar es Salaam.

“Kwa sasa niko Kahama na Agosti 23 kuna mashindano ya baiskeli na tarehe 26 nitakuwa Dar na siku inayofuata ndio nitawasilisha ripoti hiyo ya Madola,” alisema Mhagama.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi