loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makocha watakiwa kuanza na timu za vijana

Fereji alisema soka bora inaanzia katika madaraja ya vijana ambao ndio unaweza kuwafinyanga na kupata kufahamu viwango vyao na si kumfundisha mchezaji aliyepevuka umri ukategemea kupata kiwango bora.

“Vijana ndio msingi mzuri wa kuanzia na si kumchukua mchezaji mkubwa ambaye anachezea vilabu vikubwa ukafikiria utafikia lengo wakati wake huyo tena umeshapita anza na vijana upate mafanikio bora ya maendeleo ya soka letu,” alisema bosi huyo wa zamani wa ZFA.

Alisema pamoja na kasoro ndogo zilizopo katika soka lao, lakini bado Zanzibar inahitaji kuwa na viwango bora vya michezo mbalimbali ikiwemo soka.

“Si rahisi kwa mchezaji wa timu ya taifa ukaanza kumfundisha kupiga mpira huyu yeye anakuwa anapewa mbinu nyingine, lakini kijana utakavyomuanzisha ndivyo utakavyokwenda naye,” alisisitiza.

Hata hivyo, aliwataka walimu hao kutumia akili zaidi katika njia za ufundishaji pamoja na kujisomea mara kwa mara ili kwenda sambamba na mabadiliko ya soka yanayotokea kila siku.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi