loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makongo yatoa dozi netiboli Feasssa

Makongo waliongoza katika robo zote kwa kufunga 55-1 na 80-2 na kuwafanya kuwa na uhakika wa kujikusanyia pointi katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja.

Katika mchezo mwingine wa netiboli, GS Gahini ya Rwanda ilijikuta ikipokea kichapo cha bila huruma kutoka kwa shule ya sekondari ya Obambo ya Kenya baada ya kufungwa 46-13.

Wakati katika mchezo wa mpira wa wavu, Kilabela ya Tanzania waliibuka mashujaa baada ya kushinda seti 3-0 dhidi ya Malakal Boys ya Sudan Kusini katika mchezo wa wavulana.

Katika mchezo mwingine wa mpira wa wavu, shule ya Masasi ya Tanzania ilichapwa 3-0 na wenzao wa Sudan Kusini.

Katika mchezo wa mpira wa mikono uliopigwa kwenye Uwanja wa ndani wa Taifa, Sega ya Kenya iliibuka na ushindi wa bao 18-12 dhidi ya Jumba ya Sudan Kusini kwa upande wa wavulana.

Nayo Makongo ilijikuta ikigalagazwa baada ya kufungwa 29-15 na Kigoma ya Rwanda katika mchezo mwingine wa mpira wa mikono kwa upande wa wavulana.

Michezo hiyo itaendelea tena leo kwa mpira wa mikono wakati timu ya Makongo itakapocheza na Sega kwa upande wa wasichana huku Isandar ya Sudan Kusini ikikwaana na Mwanakwerekwe ya Zanzibar katika mchezo mwingine wa mikono kwa wasichana.

Kwa wavulana leo, Iyunga ya Mbeya Tanzania itachuana na Bor ya Sudan Kusini katika mchezo mwingine wa mpira wa mikono.

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi