loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makongoro Nyerere ahimiza umoja, mshikamano

Kauli hiyo aliitoa juzi kijijini Butiama, baada ya wazee kutoka mikoa ya Tanzania bara na Visiwani kutembelea nyumbani kwa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 15 ya kifo chake.

Makongoro ambaye ni mtoto wa tano wa Baba wa Taifa, alisema lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere lisiwe sifa ya maneno, bali kusimamia mambo yote mazuri aliyoyaacha kama mwongozo wa maendeleo ya nchi.

“Nimefurahishwa na wazee kumkumbuka mzee mwenzao ambaye amewatangulia mbele ya haki...moyo kama huu ni moja ya dira sahihi ambazo Mwalimu alizitumia kuwaunganisha Watanzania wote, nakumbuka wakati wa Mwalimu hakuna mtu aliyebaguliwa wala kuonewa, alihakikisha kila Mtanzania anaifurahia nchi yake,” alisema.

Awali, wazee walitoa tamko la kukemea baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kukejeli waasisi wa taifa.

Akisoma tamko la wazee hao, Cosmus Kasangai kutoka Mkoa wa Tabora, alisema azimio lao ni kukemea vikali vitendo hivyo. Walitaka serikali kuhakikisha inawachukulia hatua watu wote wanaojiusisha na kuwatusi waasisi wa taifa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Butiama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi