loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malezi yasababisha ongezeko la wagonjwa wa akili

Hayo yalibainishwa leo na Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Psychiatrist), Praxeda Swai wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Madaktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili na Wanasaikolojia kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam.

Dk Swai ambaye ni Rais wa Jumuiya ya Madaktari Bingwa na Wanafunzi wa Afya na Magonjwa ya Akili katika nchi zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki (EAYPTA) alisema vitendo vya unyanyasaji watoto na migogoro ya ndoa ndani ya jamii imeendelea kuwa sababu kubwa inayopelekea kujenga dhana ya utukutu na hatimaye ongezeko la magonjwa ya akili kwa vijana.

“Ifahamike unyanyasaji wa aina yoyote kwa watoto ikiwemo kuwapiga, wazazi kukaa mbali na familia au kumuachia mwingine akulelee mtoto wako kwa kigezo cha ajira yako...na matumizi hasi ya teknolojia kunachangia kuporomoka kwa maadili na kuzidisha matatizo ya kisaikolojia kwa kundi hilo,” alisema Swai.

Alifafanua kuwa yapo matatizo mbalimbali ya kisaikolojia yanayoweza kusababisha magonjwa ya akili kwa mfano mtu aliyebakwa, mtu aliyefikwa na majanga, mtu aliyepata ajali siku za nyuma, mikwaruzano katika ndoa, ugumu wa maisha na mahangaiko mbalimbali yanaweza kuchangia mtu kupata maradhi ya akili.

Alisisitiza kuwa ili kuboresha afya ya akili, wazazi wanapaswa kuchukua jukumu la kuwapatia malezo bora vijana wao hususan watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 6 sanjari na kustawisha uhai wa familia ili kunusuru kundi la watoto na vijana kujiingiza katika vitendo viovu na matumizi ya dawa za kulevya ambazo ni miongoni mwa vyanzo vya magonjwa hayo.

EAYPTA imeandaa mkutano huo wa siku mbili nchini ili kutathmini na kujadili maboresho ya huduma ya afya na magonjwa ya akili kwa watoto na vijana kwa kushirikisha kundi la madaktari vijana wa sekta hiyo kutoka nchi wanachama za Kenya, Uganda, Ethiopia, Somalia, Sudan, Djibout, Rwanda na Tanzania.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi