loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malinzi mgeni rasmi tuzo ya makocha

Akizungumza na gazeti hili jijini, Ofisa Mtendaji wa tuzo hiyo, Fredrick Luunga alisema Kamati ya Maandalizi ya tuzo iliyokutana hivi karibuni ndiyo iliyopitisha jina la Malinzi kuwa mgeni rasmi siku hiyo.

Luunga alisema lengo la kumwalika kiongozi huyo wa juu wa soka ni kuthamini mchango wake katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini na pia kumpa fursa ya kukutana na kuzungumza na makocha wa mpira wa miguu Tanzania na wadau wengine kupitia hafla hiyo.

Kuhusu maandalizi ya tuzo hiyo kiujumla, Ofisa huyo alisema yanakwenda vizuri na kwamba wapo katika mchakato wa kutafuta wadhamini zaidi. “Maandalizi yanakwenda vizuri na Kamati imekuwa ikikutana mara kwa mara kwa lengo la kupanga mikakati mbalimbali,” alisema.

Hata hivyo, Luunga ametoa mwito kwa wafadhili wa michezo nchini kujitokeza na kudhamini tuzo hiyo itakayokuwa ikitolewa kila mwaka.

“Bado tunahitaji wafadhili zaidi ili kufanikisha utoaji wa tuzo hizo kwani lengo ni kuhakikisha makocha wa soka nchini wanathaminiwa kutokana na kazi zao wanazofanya katika taaluma ya ukocha”, alisema.

Wakati huo huo, ofisa huyo alisema zoezi la kuwapigia kura makocha wanaostahili kupata tuzo hizo linaendelea kwa kuandika katika simu neno sokafasta acha nafasi kisha jina la kocha yeyote na tuzo anayostahili kupata kisha itumwe kwenda 15678.

Tuzo zinazotarajiwa kutolewa siku hiyo ni kocha bora wa mwaka 2013, kocha bora wa makipa, kocha bora mkongwe mwenye mafanikio, kocha bora chipukizi, kocha bora wa kike, kocha bora wa kigeni, kocha bora wa kigeni aliyewahi kupata mafanikio nchini na kocha bora Mtanzania anayefundisha soka nje ya nchi kwa sasa.

KLABU ya Chelsea imemtangaza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi