loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malkia netiboli Umisseta kujulikana leo

Kanda ya Dar es Salaam ilikata tiketi ya kucheza fainali baada ya jana kuikandamiza Magharibi kwa mabao 61-30 katika mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha mjini hapa.

Katika mchezo huo washindi tangu mwanzo walionekana kuwa moto mkali baada ya kushinda katika robo ya kwanza kwa bao 18-6 huku wakiendelea kuwa mbele kwa 32-12 wakati wa mapumziko kabla ya kushindwa 44-20 katika robo ya mwisho.

Kwa upande wa Mashariki wenyewe waliibuka kifua mbele baada ya kuichapa Nyanda za Juu Kusini kwa bao 63-34 huku Nyanda za Juu Kusini ikiongoza robo ya kwanza kwa kuwa mbele kwa mabao 8-6 lakini walishindwa kulinda ushindi huo.

Mashariki waligangamala na kuibuka na ushindi wa mabao 31-16 hadi kipindi ca kwanza kinamalizika kabla ya kuondoka na ushindi wa 55-23 robo ya nne ilipomalizika na kuwafanya kutinga fainali.

Kwa upande wa soka la wanawake, timu ya Kaskazini Mashariki ilitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Kanda ya Kati baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na Asha Shabani na Mwamvita Mohamed, ambao kila mmoja alifunga mawili kabla ya Magreth Andrew kufunga moja na kuhitimisha idadi hiyo ya mabao.

Katika mpira wa mikono kwa wavulana, Nyanda za Juu ilidhihirisha ubabe baada ya kuichapa Kanda ya Ziwa kwa bao 40-35 na kutwaa ushindi watatu huku viongozi wa Ziwa wakilalamikia waamuzi wakidai kuwa waliwabeba wapinzani wao.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi