loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mama Salma aasa wenye fistula kuwahi hospitalini

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na mke Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM katika matawi ya Mkoimba, Ng’apang’apa, Mbuyuni B, Mkanga, Mtutu na Rutende.

Mama Kikwete alisema ugonjwa wa fistula unatokana na uzazi, mwanamke akishikwa na uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu kibofu cha mkojo huharibika na mgonjwa hutokwa na haja ndogo mara kwa mara bila kutegemea.

“Mnapoona katika jamii yenu kuna mwanamke ana tatizo hili, muwasiliane na uongozi wa wilaya ili tuweze kumsaidia mama huyu kwa kumpeleka Hospitali ya CCBRT ambako atafanyiwa upasuaji na kurudi katika hali yake ya kawaida kama alivyokuwa zamani”, alisema Mama Kikwete.

Kuhusu ugonjwa wa saratani, aliwasisitizia viongozi hao kuwa wajumbe wazuri ili wawahimize wanawake kujitokeza kwa wingi kupima saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwani akinamama wengi wanakufa kutokana na ugonjwa huo kwani unatibika endapo mgonjwa atawahi kupata matibabu.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Anna Nkinda, Lindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi