loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man City kuanza na Newcastle

Kikosi cha Louis van Gaal Manchester United kitakuwa mwenyeji wa Swansea na timu ya Ronald Koeman Southampton itakuwa mgeni wa Liverpool.

Uwanja wa Celtic utakuwa ukitumika kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola, hivyo mechi yake ya ligi ya Scotland dhidi ya Partick Thistle iliyopangwa kuchezwa Agosti 9 imesogezwa mbele, lakini siku hiyo Rangers itacheza na Hearts kwenye Championship.

Kusogezwa kwa mechi Celtic Park inamaanisha kuwa klabu hiyo haitacheza ligi kuu mpaka Agosti 13 itakapokuwa mgeni wa mshindi wa Kombe la Scotland St Johnstone.

Aidha Wolves itacheza na Norwich katika mechi nyingine ya Championship huku Cardiff ikicheza na Blackburn.

Yeovil na Doncaster zitakutana kwenye League One, ambapo Fleetwood Town pia itacheza na Crewe kwenye uwanja wa Highbury.

Kwenye League Two, Luton itaanza kwa safari ndefu ndidi ya Carlisle baada ya kukosekana kwenye ligi kwa miaka mitano, huku Cambridge ilicheza na Plymouth.

Tottenham itaanza maisha chini ya kocha mpya Mauricio Pochettino kwa kucheza na West Ham, huku kocha mwingine mpya kwenye Ligi Kuu Alan Irvine akiwa na timu yake West Brom nyumbani kuikabili Sunderland.

Arsenal, iliyomaliza ukame wa miaka tisa bila taji kwa kutwaa Kombe la FA msimu uliopita, itaanza kampeni za Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi