loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Maonesho ya Biashara ya Tiba Asili ya Mwafrika

Maonesho hayo yatakayofanyika nchini kwa mara ya kwanza yameandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo, Boniventure Mwalongo, wadau mbalimbali wa tiba asili na tiba mbadala wanatarajia kushiriki katika Maonesho hayo.

Mwalongo alisema washiriki hao ni pamoja na watabibu wa tiba asili, watengenezaji wa dawa asili, wakunga wa tiba asili, kampuni za dawa asili na vipodozi vya dawa asili, wasambazaji wa tiba asili na tiba mbadala, watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na tiba mbadala.

Aidha, Mwalongo alisema wanaendelea na taratibu za kufanya maongezi na wadhamini mbalimbali ambapo watatoa taarifa rasmi baada ya kufikia tamati ya maongezi, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba nzima ya maonesho hayo.

Wadau wasiopungua 280 wameonesha nia ya kushiriki.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi