loader
Picha

Maonesho ya utamaduni wa Tanzania Mei 21

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (Tan-Trade), Jacqueline Maleko alisema maonesho hayo yataanza Mei 21 hadi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Alisema maonesho hayo, yatatoa fursa ya kuonesha vitu mbalimbali vya utamaduni wa Tanzania kama vyakula, mavazi na viungo ambapo ameongeza, “Tumeona jinsi vitu asilia vimekuwa moja ya vichocheo katika kukuza uchumi katika nchi, hivyo tumeamua kufanya maonesho hayo ili kujitambulisha kitaifa na tunalenga yawe ya kimataifa”.

Alisema maonesho hayo yatashirikisha taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Habari, Mtandao wa Biashara Tanzania (Tan-Tanzania) na Tan-Trade.

Hata hivyo, alisema kuwa mbali na taasisi hizo pia watawashirikisha na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo wazalishaji mbalimbali nchini watapata kuhakikiwa bidhaa zao asilia kama zitakuwa na viwango vya kimataifa.

HAIKUWA jambo rahisi kwa Tanzania, kujadiliana na kampuni kubwa duniani ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi