loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Marais watano, wawekezaji 350 kutua nchini

Wakuu hao wa nchi kutoka Ukanda wa Afrika Mshariki, wataambatana na wawekezaji wapatao 350. Marais wa sasa wa nchi hizo ni Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunziza wa Burundi na Joseph Kabila wa DRC.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema Tanzania ni mwenyeji wao ambao pia ndiyo imepata heshima ya kuandaa mkutano huo.

Alisema baada ya marais hao kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, watapata fursa ya kukagua vikundi vya burudani vya ngoma na matarumbeta vilivyoandaliwa kwa ajili yao.

Aidha, alisema watalakiwa na akina mama wapatao 300 walioandaliwa kutoka katika halmashauri za manispaa za mkoa huo.

“Marais hao watano watashiriki kwenye mkutano wa wawekezaji, utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Machi 25 hadi Machi 26 mchana,” alisema.

Alisema Machi 26 mchana wanatarajia kwamba wageni hao watatembelea Bandari ya Dar es Salaam, ili kuona namna nchi hizo tano za Ukanda wa Afrika Mashariki zinavyoshirikiana katika masuala ya ushuru wa forodha na usafirishaji bidhaa mbalimbali.

Pia alisema siku hiyo wageni hao watapata fursa ya kutembelea Reli ili kujionea namna ambavyo wanashirikiana nao katika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka katika nchi zao.

“Tunawaomba radhi kutokana na usumbufu utakaojitokeza kwa kipindi hiki ambacho ugeni huu utawasili hapa nchini mpaka utakapoondoka Machi 26 kutokana na baadhi ya barabara kufungwa kwa ajili ya misafara ya viongozi hawa wakuu wa nchi,” alisema.

Alizitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kuwa ni Nyerere, Kamata, Relwe, Gerezani, Sokoine na Kilwa kuelekea Bandari ya Dar es Salaam. Ugeni huo utaondoka nchini Machi 26.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi