loader
Dstv Habarileo  Mobile
Masaburi: Wanawake, vijana changamkieni uongozi

Masaburi: Wanawake, vijana changamkieni uongozi

Wito huo ulitolewa mapema jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Dk Didas Masaburi. Alisema hayo wakati akizindua mradi wa ushirikishwaji wa wanawake na vijana kwenye uongozi katika serikali za mitaa, ulifanyika katika mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang mkoa wa Manyara.

Alisema ALAT inataka kuimarisha demokrasia katika ngazi ya serikali za mitaa na huu ni wakati muafaka wa kushirikisha wanawake na vijana katika nafasi za uongozi katika utoaji wa maamuzi ili kukuza demokrasia.

“Demokrasia ya kweli hutengeneza mazingira ya maamuzi yanayoleta manufaa kwa makundi yote ya kijamii, hali hii huunda mshikamano, uelewano, undugu baina ya jamii na jamii na hivyo kupunguza malalamiko na misuguano isiyo ya lazima baina ya wanaoongozwa na wanaongoza,” alisema Dk Masaburi.

Aidha, Masaburi alisema makundi haya mawili ni muhimu kwenye maendeleo ya jamii na taifa, kwa kuwa nguvu kazi kubwa ya uzalishaji ipo kwa wanawake na vijana.

Alisema wanawake na vijana wakishirikishwa katika uongozi na kupewa fursa ya kuchangia katika maamuzi, itasaidia kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Masaburi alisema kuwa kwa kuanzia, mradi huo utatoa mafunzo hayo kwa Halmashauri ya wilaya za Hanang, Babati na Manispaa ya Mtwara.

Matokeo yatakayopatikana katika wilaya hizo, yatasambazwa katika halmashauri zote nchini ili kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa mwakani.

Mradi huo wa miezi 18 ni matokeo ya mafunzo yanayotolewa na kituo cha kimataifa cha ukuzaji wa Demokrasia katika Serikali za Mitaa cha Sweden, ambacho hutoa mafunzo kwa watendaji na viongozi katika serikali za mitaa.

RAIS wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amesema wakati umefika kwa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Manyara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi