loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mashabiki kuchagua uenyeji Pasaka

Mfumo huo utasaidia mashabiki wa mikoani kuteua mikoa yao ifikiwe na tamasha hilo la kumuimbia na kumtukuza Mungu kupitia nyimbo na mapambio kupitia nyimbo mbalimbali.

Wakati taratibu za maandalizi zikiendelea, Kampuni ya Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo hivi sasa wanasubiri kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama bado tunasubiri Basata watukabidhi kibali cha kufanikisha tamasha hilo ambalo mikoa sita imeonesha nia ya kuandaa tamasha hilo.

Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga kusikiliza mikoa mingi zaidi kwa sababu inaonekana mikoa mingi ina kiu ya kupata neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.

Alisema wako kwenye mchakato wa kuandaa mfumo utakaofanikisha mikoa kujipigia kura.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi