loader
Picha

Mashindano ya baiskeli Geita yafikia tamati

Mashindano hayo yaliyoendeshwa katika mtindo wa makundi, yalifikia kikomo huku washindi mbalimbali wakipatikana kutokana na raundi walizokimbia katika mashindano hayo yaliyofana kuanzia siku ya ufunguzi mpaka kufika kilele chake wiki hii.

Katika Kundi A, washindi walikuwa Hamisi Mwigulu, Hamisi Kipili, huku bingwa wa mbio za baiskeli zaVodacom, Mhindi Ngw’igi kutoka Shinyanga akishika nafasi ya tano katika kundi hilo ambalo walikimbia raundi 130.

Washindi wa Kundi B ambao walizunguka raundi 75 ni Kulwa Kipili, Masanyenge Lita na Shiku wale. Kundi C washindi walikuwa ni Ndalanhawa Gerard, Ruhende Lasi, Bureji Dede, Hatarai John, Sagharani Marunde waliokimbia raundi 67 kuzunguka uwanja.

Mashindano hayo yalijumuisha washiriki 28 kutoka mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga.

Kwa upande wake, Mratibu wa mashindano hayo Raphael Ngeleja alisema mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya baiskeli yanayotarajiwa kufanyika Shinyanga mwezi huu.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi