loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mashine za umeme Kidatu kukarabatiwa

Ziara hiyo ya waandishi wa habari kwa mujibu wa Lyaruu, ililenga kuwaonesha miradi mbalimbali ya Tanesco ambayo mwishoni mwa mwaka huu inaadhimisha miaka 50 tangu shirika hilo lianzishwe.

“Kama mnavyoona kuna mashine zimezeeka, kama hizi za kukata umeme, tangu mtambo ulipotengenezwa mwaka 1970 hazijawahi kufanyiwa ukarabati hivyo tunaona sasa ni wakati mwafaka kuzifanyia ukarabati,” alisema Lyaruu.

Aliendelea kusema, “Mbali na hivyo vikata umeme, pia kuna vitu vingine vya kukarabati kama mfumo wa mashine za hewa kwenye mgodi , kuna mabomba, pampu zimekwisha, zinatakiwa kufanyiwa ukarabati vinginevyo zitaharibika zaidi na maji yatarudi mtoni badala ya kupita njia yake ya kawaida kwenye kutengeneza umeme.”

Mtambo wa kufua umeme wa Kidatu ulijengwa mwaka 1970 kwa awamu tatu na kukamilika mwaka 1988. Tangu ulipokamilika, ulifanyiwa ukarabati mara mbili; mwaka 1993/1994 ambapo ukarabati ulikuwa mdogo na mwaka 1999 hadi 2003 ulifanyika ukarabati mkubwa.

Kuhusu hali ya ujazo wa maji kwenye bwawa, Lyaruu alisema lina maji ya kutosha hivyo hakutarajiwi kuwa na tatizo la umeme kwa siku za karibuni.

“Tuna uzalishaji wa maji wa kutosha, kwa mfano kwa leo (juzi) ujazo ni mita 449 ambao ni wa kawaida na unamudu kwa shughuli za kuzalisha umeme, mvua za masika zilizopita zilitusaidia sana,” alisema.

Bwawa la Kidatu ndiko kwenye mitambo mikubwa inayozalisha umeme kwa ajili ya gridi ya Taifa kwa kutumia maji. Kwa mujibu wa Meneja huyo, mitambo hiyo inazalisha na kuchangia uniti 450 katika gridi ya Taifa.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Kidatu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi