loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mata atua Man United, Wenger ang’aka

Mchezaji huyo wa zamani wa Valencia alikuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa misimu miwili baada ya kuhamia Stamford Bridge, Agosti 2001, lakini amejikuta hana nafasi katika kikosi cha Jose Mourinho tangu aliporejea klabuni hapo msimu huu.

Na Wenger anaamini Mata ameruhusiwa kuhamia Old Trafford kwa sababu Chelsea tayari imeshacheza na United mara mbili katika Ligi Kuu msimu huu, na karibuni ikishinda mabao 3-1, Jumapili iliyopita.

“Ndiyo, nimeshangaa kwa sababu Juan Mata ni mchezaji mahiri, na wao (Chelsea) wanauza mchezaji mahiri kwa mpinzani wao moja kwa moja,” alisema Wenger.

“Inatoa fursa katika soko la uhamisho kwa sababu Chelsea tayari imecheza mara mbili dhidi ya Man United na kwa hiyo hawatacheza nao tena.

“Baadhi ya timu zimecheza mara mbili dhidi ya timu moja pinzani na baadhi bado, na nafikiri kama unataka kuheshimu haki kwa kila mmoja, hilo halipaswi kufanyika.

“Nafahamu kiundani nini wanachofanya Chelsea, iko ndani ya sheria, lakini labda sheria zinapaswa kutekelezwa kwa haki.”

Arsenal ambao wanaongoza Ligi Kuu watacheza na Chelsea na United miongoni mwa mechi zao 16 zilizobaki msimu huu, huku United ikiwa ya kwanza katikati ya mwezi ujao.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi