loader
Picha

Mataifa mengine yaige China nafasi za masomo

Hivyo, kwanza tunaipongeza na kuishukuru serikali ya China na tuna imani itaendelea kuisaidia Tanzania, kama ambavyo imekuwa ikifanya hivyo.

Pili, tumefurahishwa na taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi kuwa Serikali ya China imeipatia serikali ya Tanzania fursa 659 za mafunzo kwa mwaka 2018 kwa ajili ya watumishi wa umma 4,812.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro, mafunzo hayo yamegawanyika kwenye makundi manne, ambayo ni kozi kwa ajili ya watumishi kutoka sekta mbalimbali, kwa ajili ya viongozi, kozi za muda mfupi na kozi za muda mrefu.

Kwa upande wa kozi kwa ajili ya watumishi kutoka sekta za usimamizi rasilimaliwatu, afya ya jamii, elimu, kilimo na utawala wa serikali za mitaa na maendeleo ya kiuchumi ina fursa sita na itahusisha watumishi 140.

Kozi kwa ajili ya viongozi, kuna fursa 30 na kushirikisha viongozi 210 ambazo zitahusisha mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi.

Kwa upande wa kozi fupi, kuna fursa 585 na zitahusu watumishi 4,095, ambao ni watumishi wa umma waandamizi na ngazi kati, wenye uzoefu na sifa za kusimamia na kufanya kazi katika sekta inayohusu kozi iliyotolewa.

Kozi za muda mrefu kwa shahada ya uzamivu na uzamili ambazo kuna fursa 38 na kuhusisha watumishi 367, ambayo itajumuisha watumishi wa umma wenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu kazini.

Fursa za mafunzo zimelenga maeneo ya kipaumbele ya taifa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa na miaka mitano ambayo inahusisha uhandisi wa viwanda, mawasiliano, usafirishaji, kilimo, elimu, afya, biashara, uchumi, tehama na utawala bora.

Mafunzo zitagharamiwa na Serikali ya China, ambayo ni gharama za usafiri wa ndege wa kwenda China na kurudi Tanzania, malazi, chakula na ada.

Waajiri watatakiwa kuwawezesha watumishi walio chini yao, kuomba na kuweza kuhudhuria mafunzo, kulingana na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Hivyo, tunaomba wadau wa maendeleo na mataifa mengine, waige mfano mzuri uliooneshwa na China katika kutoa fursa nyingi na mbalimbali za masomo kwa Watanzania.

WATANZANIA juzi walikesha wakishangilia baada ya timu yao ya soka ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi