loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Matumaini Reli ya Kati yaonekana

Mabehewa yaliyopokewa jana jijini Dar es Salaam ni ya kubebea kokoto, ambayo yametoka India huku yakielezewa kuwa ni miongoni mwa vitendea kazi muhimu katika mkakati mzima wa kuboresha reli hiyo ya kati.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliyepokea mabehewa hayo, alisema mwanzoni mwa mwaka ujao, Reli ya Kati itakuwa imeimarika kwa ajili ya kuwezesha, siyo tu usafiri wa abiria, bali pia mizigo.

Alisema mabehewa hayo yenye thamani ya Sh bilioni 4.316, yatatumika kwa kubeba na kusafirishia kokoto kutoka sehemu zinakozalishwa na kupeleka kwenye maeneo kwa ajili ya kushindilia reli wakati wa matengenezo ya njia hiyo.

“ Hii itasaidia kuimarisha njia ya reli na kuwezesha kupitisha mizigo na abiria kwa usalama zaidi. Ni matarajio yangu TRL watayatumia vizuri ili yaweze kutumika kwa muda ujao,” alisema.

Akizungumzia huduma duni inayotolewa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mwakyembe alisema: “Ni lazima TRL ishindwe kutoa huduma nzuri kwa sababu haina vifaa na huwezi kuwalaumu. Kwa hali iliyopo kulikuwa na njia mbili; kusimamisha kabisa huduma au kuimarisha.”

“Mwaka 2002, TRL ilikuwa na vichwa zaidi ya 50 na mabehewa 2,200, leo tunaongelea vichwa vya treni vinane na mabehewa chini ya hapo, sasa vichwa vinane kutumika kwa treni ya mizigo na abiria hakutaweza kuwa na ufanisi,” alisema.

Waziri Mwakyembe alisema serikali imejipanga kuhakikisha Reli ya Kati, inaimarika kwa kuagiza vifaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vichwa vya treni na mabehewa ya mizigo na abiria.

Alisema kati ya Agosti na Desemba, itapokea mabehewa ya mizigo 274, mabehewa ya breki 34 na mabehewa 22 ya abiria.

Mwakyembe alisema kati ya Januari na Mei mwakani, serikali itapokea vichwa vya treni vipya 13, chini ya mradi unaotekelezwa na Kampuni ya EMD ya Marekani.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi