loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mawakala walivyo ‘shubiri’ kwa wakulima wa mahindi

Kutokana na hilo Serikali imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali katika kukwamua kilimo na wakulima, ili kilimo kiwe na tija na pia wakulima waweze kunufaika na kazi yao.

Juhudi hizo zimeongeza ari hadi kuwa na ongezeko la uzalishaji hivyo serikali kuja na mfumo wa kununua nafaka kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wenye lengo la kuhifadhi chakula cha kusaidia upungufu wa chakula na kusimamia biashara kama wakala.

Kupitia mfumo huo, wakulima wananufaika na bei nzuri ya mazao yao inayotolewa na NFRA. Kwa mfano, tangu kuanzishwa kwa NFRA, bei ya kilo moja ya mahindi imekuwa Sh 500 hivyo kufanya gunia moja lenye kilo 100 kuuzwa kwa Sh 50,000 ikiwa ni bei ya juu tofauti na walanguzi ambao walikuwa wakinunua kati ya sh 20,000 hadi 30,000.

Lakini juhudi hizo zinaingia dosari kutokana na wajanja wanaotumia nafasi hiyo kuendelea kuwanyonya wakulima wakiwamo watendaji wa NFRA.

Kupitia ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana ambaye amefuatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiwa na kazi ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani na ahadi za chama hicho sambamba na kuimarisha chama ambayo wanaifanya katika mikoa ya pwani, Tanga na Iringa imebainisha kuwa pamoja na juhudi za serikali bado wakulima wanadhulumiwa.

Kupitia mtindo wake mpya wa mahakama ya wazi, ambayo inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kutoa kero zinazowasumbua hivyo wahusika kujibu hoja hizo na kutoa maelekezo ya ufuatiliaji pale inapobidi. Kupitia mahakama ya wazi, wananchi wameweza kubainisha jinsi wakulima wanavyodhulumiwa na wajanja wachache ambao wanatakiwa kumulikwa ili wakomeshe tabia hiyo.

Kilio cha dhuluma ya wakulima kilianzia wilayani Handeni ambapo Fadhil Juma anasema Serikali kwa nia nzuri iliona wananchi hususan wakulima wanapata tabu na soko la mazao na kutapeliwa hivyo kuanzisha vituo vya kununua mahindi.

“Leo yule mkulima aliyelengwa na serikali, hawezi kupata msaada wa mahindi yake kununuliwa, bali matapeli wanakwenda kwa wakulima na kununua kwa bei ya kuwalalia na wanakwenda kuyauza kwenye vituo vilivyowekwa na serikali kwa bei nzuri, mwisho wa siku mkulima hapati chochote na anaendelea kuwa masikini,” anasema Juma.

“Ukienda na mahindi yako pale katika kituo unachengwa chengwa kwa kuambiwa mahindi ya Kilindi hayatakiwi yanatakiwa ya Kiteto, wakati serikali iliweka vituo hivyo, ili wananchi wanufaike na kupata kipato,” anaongeza Juma. Kilio hicho kilichokuwa kikitolewa mbele ya Kinana kikafika Wilaya ya Kilindi ambapo wananchi wanalalamikia urasimu pamoja na rushwa katika ununuzi wa mahindi katika soko lililoanzishwa Songe, wilayani Kilindi kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete.

Wakulima hao walimweleza Kinana kuwa soko hilo halinufaishi wakulima wadogo kama alivyoagiza Rais Kikwete bali wafanyabiashara wakubwa. Mwajuma Nassoro anasema madalali wameonekana kuwa chanzo cha kuvuruga utaratibu wa ununuzi wa mahidi unaofanywa na NFRA na kuwakosesha haki ya kuuza kwa wakulima wadogo ambao ndio walengwa.

“Imekuwa vigumu kwa mkulima kuuza mahindi katika soko la mahindi la Songe, kutokana na kuwapo urasimu, rushwa na madalali ambao wamekuwa wakiwafanyia kazi wafanyabiashara wakubwa. “Ukifika sokoni ili uuze, lazima uwe na gunia tupu za serikali ambazo hutumika kuuzia mahindi, lakini utakuta dalali mmoja amechukua gunia zaidi ya 100 kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa, sasa wewe ukija na gunia moja wala huwezi kuuza mahindi yako,” amesema.

Naye Masudi Salum alisema kukithiri kwa rushwa katika soko hilo la mahindi la Songe ni jambo ambalo linawanufaisha wafanyabiashara wakubwa ambao hununua mahindi kwa bei ya chini kutoka kwa wakulima walioshindwa kuuza mahindi yao katika soko hilo na wao kuyauza kwa NFRA ambayo hulipa bei kubwa kuliko wao.

“Watu wanaokuja na malori mawili au matatu ndio wanaopewa kipaumbele na hao watendaji wa NFRA. Sasa kwa sababu mimi ninashida na siwezi kusubiri muda mrefu wa kuuza mahindi nalazimika kuwauzia wafanyabiashara hao,” anafafanua Salum.

Kutokana na malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, anakiri kuwa urasimu na rushwa katika soko hilo unarudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuwa juhudi walizofanya ni kuwasiliana na Taa- sisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

“Malalamiko yaliyotolewa ni sahihi nasi tuliyapata. Soko lilipoanza kikao cha makubaliano baina ya mnunuzi pamoja na wananchi na viongozi wa kata, ilikuwa tani 100 zinunuliwe kwa wakulima wadogo, ingawa hili linaonekana halitekelezwi,” anasema Salum. Anaongeza: “ Lakini kuna tatizo ambalo limejitokeza, wakulima wadogo wakipima mahindi yao wanarudishwa kuwa mahindi hayajakauka ipasavyo au machafu, na watu hao hao wanamzungukia mkulima na kuyanunua kwa bei ya chini.”

Katika mavuno ya mwaka huu kuna ziada ya tani 5,000 za mahindi na zilizokuwa zimenunuliwa ni tani 2,000 tu. Kwa malalamiko hayo, Kinana anamuagiza Mkuu wa Wilaya Selemani Liwowa kuhakikisha anashughulikia malalamiko hayo ili lengo la kuanzishwa kwa soko hilo liwe na manufaa kwa wakulima.

“Mwezi Julai Rais (Jakaya Kikwete) alifanya ziara na wananchi walimlalamikia kukosekana kwa soko la mahindi na ndipo alipomuagiza Waziri wa kilimo na chakula kuweka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kununua mahindi hapa, sasa nakuagiza DC simamia hili ili soko liwe na manufaa kwa wakulima,” anafafanua Salum.

Kinana anaahidi wananchi kuwa atawasiliana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza ili kutatua kero hizo na kununua mahindi yaliyobaki. Liwowa anasema: “Maelekezo yako wanayapokea na tutaendelea kuyafanyia kazi ili wakulima wanufaike na soko hili ambalo lilijengwa baada ya wananchi kumsimamisha rais na kumlalamikia kukosekana kwa soko,” alisema.

“WANAOFANYA shughuli za maendeleo katika vyanzo vinavyotiririsha maji ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi