loader
Picha

Mawakili kusomea sheria za gesi, mafuta Marekani

Hayo yalisemwa jana na makamu wa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika, Flaviana Charles wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema chama hicho pamoja na majukumu mengine, kina jukumu la kusimamia upatikanaji wa elimu ya sheria hivyo ushirikiano huo wa kuwapatia mawakili mafunzo ni njia mojawapo ya kuboresha, kusimamia na kuwaongezea mawakili ujuzi na uwezo wa kulinda haki na usawa katika jamii.

Alisema mafunzo hayo yatakuwa ni ya miezi mitano yatakayoanza Septemba mosi mwaka huu na kutarajiwa kumalizika Januari mwakani na watasoma masomo matatu ambapo somo mojawapo la lazima kusoma ni somo la mafuta, na gesi na madini.

Rais wa The Colom Foundation INC na Nashera Hotel, Wilbur Colom ambaye ni mwekezaji hapa nchini, alisema mafunzo hayo hadi kumalizika yatagharimu kiasi cha dola 12,500 (Sh milioni 20.3) kwa kila mwanafunzi, hivyo wao kama wawekezaji watahusika moja kwa moja katika kuleta maendeleo katika nchi waliyowekeza na kuwa wanajiona ni sehemu ya Taifa.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi