loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maximo ateta na Kaseja

Maximo ambaye leo asubuhi ataanza rasmi kukinoa kikosi cha Yanga kwenye fukwe za Coco, alikutana na wachezaji hao ili kutaka kufahamiana nao na kuweka mikakati kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ujao pamoja na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kuanza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mmoja wa wachezaji wa Yanga, Maximo alizungumza mambo mbalimbali ya kimkakati kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ambayo watashiriki, lakini pia alimhakikishia Kaseja kumaliza tofauti zao na kuwa na ushirikiano katika kuipa mafanikio Yanga.

“Kweli leo tumekutana na kocha kwa mara ya kwanza hapa klabu na amezungumza mambo mengi ya kimkakati, lakini pia amemhakikishia Kaseja nafasi katika timu na kumtaka wasahau yaliyopita, wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuipa mafanikio Yanga,” alisema mchezaji huyo aliyehudhuria kikao na Maximo.

Mchezaji huyo alisema baada ya mazungumzo hayo, Maximo alimtaka Kaseja kubaki ili wazungumze wakiwa wawili akiwa kama mchezaji mkongwe na mwenye uzoefu ambaye anaweza kumsaidia katika mipango yake ya kuifanya Yanga ipate mafanikio msimu ujao.

“Baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja, kocha alimchukua Kaseja na kukaa naye pembeni wawili tu na walizungumza kwa muda mrefu nadhani ilikuwa ni kumaliza hizo tofauti zao zilizokuwepo kabla hajaondoka,” aliongeza mchezaji huyo.

Maximo aliyerejea nchini Jumanne iliyopita na kuingia mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Yanga, aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars kati ya mwaka 2006 hadi 2010, ambako hakuwa na uhusiano mzuri na Kaseja na alimwacha katika kikosi chake baada ya kucheza kwa muda mfupi.

Jumatano iliyopita, Maximo alitangaza hadharani kumaliza tofauti yake na kipa huyo aliyekwaruzana naye wakati akiifundisha timu ya taifa mwaka 2008.

Inadaiwa kuwa raia huyo wa Brazil alikerwa na Kaseja kuchekelea kitendo cha kipa mwenzake, Ivo Mapunda kufungwa mabao 4-0 na Senegal katika pambano la michuano ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika lililochezwa Dakar, kitendo ambacho kocha huyo alikitafsiri ni kukosa uzalendo.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi