loader
Picha

‘Mazingira ya uwekezaji sasa ni rafiki’

Kauli hiyo ilitolewa leo Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa.

“Nawasihi wajasiriamali katika mambo ya Tehama ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa nje ya nchi ili waweze kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu,” alisema Mbarawa.

Mbarawa alisema Tanzania inakaribisha wawekezaji kwenye Tehama kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini hadi vijijini.

Alitaja changamoto zinazoikabili Sekta ya Tehama ni pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa vifaa vya sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi, Tharcisse Nkezabahizi alisema Tehama ni moja ya nyanja muhimu inayotumiwa katika nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network la nchini Finland, Cipa Ojala alisema mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambao nchi nyingi zinatumia fursa iliyopo ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analojia kwenda dijiti.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Eleuteri Mangi- MAELEZO

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi