loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbaroni kwa kuwaua, kuwang’oa meno tembo

Fidelis Kikungwe (40) ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Kidayi, anadaiwa kufanya mauaji hayo ya wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, katika taarifa yake jana kwa waandishi wa habari, alisema mtuhumiwa alitiwa mbaroni Julai 26, mwaka huu saa 11:30 jioni.

Alisema alikamatwa kutokana na juhudi za polisi na wananchi wa kitongoji hicho kusaka watu wanaodaiwa kuendesha vitendo vya ujangili baada ya taarifa kulifikia jeshi hilo. Alisema wanaendelea kusaka mtandao wa majangili.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, wananchi wa eneo hilo baada ya kusikia milio ya risasi Julai 22, mwaka huu saa 12 jioni, walikusanyika na kufuatilia tukio hilo. Inasadikiwa wahusika wa ujangili walipata hofu wakatoweka.

Kamanda alisema kulionekana tembo wawili wote madume wakiwa wameuawa na kung’olewa meno manne yaliyofichwa kwenye majani kwenye msitu huo.

Kwa mujibu wa Polisi, katika kumhoji mtuhumiwa alikiri kuhusika na ujangili huo na katika ufuatiliaji alionesha silaha iliyotumika kuua tembo hao.

Silaha hizo ni Rifle 375 yenye namba TZ 43818 NP 19 na meno manne ya tembo pamoja na shoka lililotumika kung’olewa meno hayo baada ya kuwaua kwa risasi.

“Aidha zipo taarifa kuwa mtuhumiwa huyu anashirikiana na watu ambao bado tunawatafuta,” alisema Kamanda.

Alisema uzito na gharama ya meno hayo vitafahamika baada ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa kupima. Alishukuru wananchi kwa kuitikia mwito wa operesheni shirikishi.

S ERIKALI imelipa fi dia ya Sh bilioni 3.2 kwa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi