loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbeya City tayari kwa mzunguko wa pili

Mwapunda alisema wiki hii walipanga kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Makonde Combine ya Zambia, lakini walishindwa kutokana na kuona muda umekwisha kwani wanahitajika kutulia ili kujiandaa kusafiri.

“Hatukucheza tena mechi za kirafiki, tumeona tusubiri kwa kufanya maandalizi mapema kwasababu wakati wowote wiki hii tunatakiwa kwenda Kagera na unajua tena kule ni mbali sana, hadi tufike na kusoma mazingira ili tujiweke vizuri,” alisema mwenyekiti huyo.

Mbeya City ilimaliza Ligi Kuu mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi 27.

Mwapunda alisema mawazo yao yote katika mzunguko huu ni kujitahidi kurudi kwa mbio zile zile walizoingia nazo awali.

Alisema kikosi chao kiko kamili na hakuna majeruhi yoyote hivyo kupitia wachezaji waliokuwa mzunguko uliopita ndio watakaocheza tena ila kuna marekebisho wamefanya kuboresha upungufu uliojitokeza awali.

Alisema lengo lao la kwanza ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na kutengeneza historia ya klabu.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi