loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mbeya City yaichimba mkwara Simba

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwapunda alisema watapeleka aibu kwa Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kujitokeza kuishangilia timu yake kwa sababu Mbeya City iko vizuri na imejiandaa kufanya mauaji na kuondoka na pointi tatu muhimu.

Mapema wiki hii, Rage alitangaza kuwa atakuwepo Mbeya kushuhudia mchezo huo dhidi ya Mbeya City, huku akitamba kuwa lazima Simba waondoke na ubingwa.

Mwapunda alisema ikiwa atakuja atapata majanga, kwani kikosi chake kipo fiti na hakuna majeruhi yeyote na kwamba wachezaji wote wako vizuri kwa ajili ya mchezo huo na wanaisubiri Simba kwa hamu kupambana nao.

“Nawaambia Simba kwamba hatuwaogopi, kwa sababu wanakuja nyumbani tumejipanga kukabiliana nao, lengo letu ni kuchukua ubingwa na kujiongezea pointi,” alisema.

Mwapunda alisema Simba lazima waondoke na aibu kama ilivyokuwa kwa Mtibwa Sugar ambapo wiki iliyopita waliwafunga bao 2-1, na kujiongezea pointi 34, ikiwa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga yenye pointi 35 huku Azam ikiongoza kileleni kwa pointi 36.

Mwenyekiti huyo alisema wanataka kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo ili kuchukua nafasi ya pili au ya kwanza. Aliwahimiza mashabiki wa Mbeya City kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuinga mkono iweze kufanya vizuri.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi