loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbeya wahimizwa kusajili majina ya biashara

Rai hiyo imetolewa mjini Mbeya na Meneja Uhusiano wa benki ya NMB, Nyanda za Juu Kusini, Focus Lubende alipokuwa akishiriki kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara waliohudhuria semina ya mafunzo inayoendeshwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Lubende alisema ni kwa kusajili biashara zao katika mamlaka za Serikali ambapo wafanyabiashara wataweza kutambulika na kuweza kupata huduma kama za mikopo na nyinginezo.

“Sajilini majina ya biashara zenu ili tuwatambue na muweze kufaidika na mikopo kuendeleza biashara zenu,” alisema.

BRELA inaendesha mafunzo kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuhusiana na kazi wanazofanya na jinsi wafanyabiashara wanavyoweza kufaidika na huduma zao.

Kwa mujibu wa Msajili Msaidizi Mwandamizi wa BRELA, Rehema Kitambi lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na wakati wa Mkoa wa Mbeya kuhusu umuhimu wa kusajili biashara zao na kusajili majina ya biashara zao.

BRELA ipo katika mchakato wa kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa kusajili majina ya biashara popote nchini na nje ya nchi kwa kutumia mtandao.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi