loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Mbunge anakwamisha ujenzi wa maabara'

Kutokana na hali hiyo baadhi ya viongozi hao wamemtaka Mbunge huyo kurudi kwa wananchi kufuta kauli yake ili ujenzi wa maabara uendelee na umalizike kama ulivyopangwa.

Wakizungumza hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatma Ally katika tarafa za Mvumi na Makang’wa kukagua ujenzi wa maabara.

Walisema walikuwa wakiendelea vizuri na ukusanyaji fedha kutoka kwa wananchi lakini baada ya Lusinde kufanya mkutano na kutangaza uchangiaji ni hiari watu waliacha kuchangia.

Walisema kauli ya Mbunge imewafanya waonekane maadui kwani wanapopita kudai michango wananchi wamekuwa wakikataa kulipa huku wakati mwingine wakifukuzwa na mapanga.

“Baada ya ziara ya Mbunge, wananchi walitaka warudishiwe fedha zilizokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa maabara sasa tunatishiwa maisha na kesi mbili ziko Polisi,” alisema mmoja ya viongozi hao.

Hata Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Ulanga alisema suala la siasa isiwe sababu ya kukwama kwa zoezi la ujenzi wa maabara.

“Lazima wananchi mchangie kwani watakaosoma ni watoto wenu na si watoto wa mbunge,” alisema.

Alisema kama Mbunge alikuwa na hoja katika hilo alitakiwa kuandika barua za kusimamisha michango ya ujenzi wa maabara na si kuishia tu kutoa maneno ambapo mwisho wa siku anaweza kukana maneno hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino alisema suala la uchangiaji wa ujenzi wa maabara si hiari ni lazima kwani hilo ni tamko la Rais linatakiwa kutekelezwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Samwel Kawea alisema kimsingi ifikapo uchaguzi wa 2015 Mbunge lazima atasema amejenga maabara ni muhimu wananchi kupima maneno kama yana tija kwa jamii. Alisema hata shule za Kata zilijengwa kwa mtindo huo huo wa ujenzi wa maabara.

“Nchi nzima shule za Kata zimejengwa kwa kutumia michango ya wananchi lazima kufuata sheria na taratibu,” alisema.

Alipohojiwa kuhusiana na kauli hizo, Lusinde alisema katika mikutano ya hadhara aliyofanya hivi karibuni katika Jimbo la Mtera alikuta watu wakiwa wamefungiwa ndani kwa saa 24 kwa kushindwa kulipa mchango wa ujenzi wa maabara.

“Wameshindwa kushawishi watu wachangie sasa wanakamata watu na kuwafungia ndani?” Alihoji.

Alisema viongozi walikuwa na wajibu wa kuelimisha watu na watendaji kuwa wachangiaji wa kwanza. “Ujenzi huu unatumia muda mfupi na matokeo wanabanwa watu wasio na uwezo,'’ alisema.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Chamwino

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi