loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge: Kuna ubaguzi ajira Polisi

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo alipokuwa akiuliza swali jana, alitaka Serikali ifanyie marekebisho sheria alizoita za zamani, ili ajira za Polisi na watendaji wengine serikalini ziwe sawa.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, alisema Serikali itaendelea kufanyia marekebisho sheria zote za hifadhi ya jamii kila inapobidi.

Alisema askari polisi anapoajiriwa kwa mara ya kwanza, hupewe Mkataba wa miaka mitatu, ambayo huongezwa muda mpaka atakapotimiza miaka 12 na wakati huo, katika akiba yake ya uzeeni Serikali huchangia asilimia 15 ya mshahara na mwajiriwa asilimia 10.

Kwa mujibu wa Mahanga, askari akishatimiza miaka 12, hupata ajira ya kudumu na katika malipo ya pensheni, Serikali huchangia asilimia 15 na wao asilimia 5.

Alifafanua kuwa mwaka 2012, Serikali ilifanyia marekebisho sheria zote za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ili ziendane na matakwa ya Sheria ya Usimamizi na Udhbiti wa Hifadhi ya Jamii ya 2008.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), alitaka kujua lini masharti ya mchango wa pensheni wa mwajiri na mwajiriwa yatalingana katika mifuko yote.

Alitoa mfano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambalo michango ya mwajiri ni asilimia 10 na mwajiriwa asilimia 10, wakati katika mashirika mengine ya hifadhai ya jamii, mwajiri huchangia asilimia 15 na mwajiriwa asilimia 5.

Akijibu hoja hiyo, Mahanga alisema suala hilo ni moja ya masuala yanayofanyiwa kazi na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na kazi hiyo ikikamilika, itawasilishwa bungeni.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Joseph Lugendo, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi