loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge Nassari kufunga ndoa kesho

Hayo yalisemwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, muda mfupi kabla hajatoa ratiba rasmi ya shughuli za Bunge kwa siku sita kuanzia jana hadi Juni 11, mwaka huu.

“Kabla sijatoa matangazo yetu ya leo, naomba kuwaeleza waheshimiwa wabunge kuwa mmoja wa vijana wetu, Nassari, atafunga harusi siku ya Jumamosi,” alisema kwa furaha Spika na kushangiliwa na wabunge kadhaa.

Haikufahamika mara moja harusi hiyo itafungwa wapi. Inaaminika kuwa Nassari ni mmoja wa wabunge wenye umri mdogo bungeni.

Wabunge wengine wenye umri mdogo ni wabunge wa Chadema, Felix Mkosamali wa Muhambwe, Highness Kiwia wa Ilemela na David Silinde wa Mbozi Magharibi.

Katika Baraza la sasa la Mawaziri Kivuli, Nassari ni Naibu Msemaji wa Upinzani wa Wizara za Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Wiki chache zilizopita, Mbunge mwingine, Vicky Kamatta wa Viti Maalumu (CCM), aliripotiwa kuwa alitarajia kufunga ndoa jijini Dar es Salaam, lakini haikuwezekana, kwa sababu aliugua ghafla.

Kwa sasa Mbunge huyo kutoka Mkoa wa Geita, amepata nafuu na amerejea bungeni.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi